IVO MAPUNDA AIGEUKA SIMBA MWISHONI, AMWAGA WINO MWAKA MMOJA GOR MAHIA.
Wakati Simba ikieleza kuwa wameshamalizana na kipa chaguo la kwanza la timu ya Kilimanjaro Stars, Ivo Mapunda, na kilichobaki ni kusaini tu, mlinda mlango huyo amekanusha vikali na kuweka wazi kuwa anasaini mkataba mpya wa kuitumikia Gor Mahia.
Ivo, ambaye ni kipa namba mbili katika klabu hiyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Kenya na akiwa ameonyesha uwezo wa hali ya juu akiwa na timu yake ya Kilimanjaro Stars, amesema anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea Gor Mahia.
Akizungumza jana, Ivo alisema tayari viongozi wake wa Gor Mahia wamemfuata na kumueleza wanataka kumpa mkataba mpya.
Kipa huyo ambaye aliwahi kuichezea Yanga na Prisons zote za Tanzania Bara, akizungumzia suala la kuzungumza na viongozi wa Simba, alisema hajawahi kufanya mazungumzo nao.
Kadhalika alisema, amefurahi kuona ameitumikia vizuri timu yake ya Kilimanjaro Stars licha ya kutofika fainali ya mashindano ya Kombe la Chalenji.
"Nitabaki Gor Mahia kwa mwaka mwingine mmoja, walinipigia viongozi wangu wakataka kuja kambini nisaini, lakini nikawaambia wasubiri nimalize mashindano ya Kombe la Chalenji," alisema kipa huyo.
Hata hivyo, kipa huyo ambaye mashabiki wa Gor Mahia wamekuwa wakiushinikiza uongozi wa timu hiyo kumsajili, hakuwa tayari kutaja dau ambalo atapatiwa na klabu yake hiyo.
Mkataba wa awali wa Mapunda na Gor Mahia unatarajiwa kumalizika Desemba 16, mwaka huu.