MESSI HATOENDA KOKOTE-ROSELL.
Staa matata wa Barcelona, Lionel Messi, hataenda popote katika utawala wa rais Sandro Rosell kiongozi huyo alitangaza Alhamisi.
"Kwa muda wote nitakuwa rais, lolote liwezekanalo au lisilowezekana litatendwa kuhakikisha Messi anasalia kitako hapa," Rosell alihimiza katika hafla ya kuwasilisha mkataba wa ushirikiano baina ya Barca na kampuni kuu ya elektroniki ya Marekani, Intel.
"Ni vigumu sana, au tuseme haitowezekana, kuwa Messi ataondoka timu hapa."
Mshindi mara nne wa tuzo la Ballon d' Or anauguza jeraha na anatarajiwa kurudi uwanjani Januari huku kandarasi yake Barcelona ikidumu hadi 2018 karibu na wakati nyota huyo atakuwa karibu kuadhimisha miaka 31 tangu kuzaliwa kwake.
Tetesi kuhusu hatima yake zilizuka Jumanne pale makamu wa rais wa maswala ya kiuchumi Barca, Javier Faus, alipofichua hakuna haja ya kujadilia kandarasi yake upya.
"Kwanini? Kandarasi yake Ilijadiliwa upya miezi sita pekee iliyopita," Faus aliambia kituo cha redio cha Rac1.
Kulingana na duru Uhispania, Messi ana kipengee cha Euro milioni 250 kwa yeyote anayetamani kumtia huru kutoka minyororo ya kandarasi yake na Barca injawaje timu zenye uwezo wa kutimiza hayo ni chache muno.
Uvumi kuhusu uwezekano wa mazungumzo mapya baina ya mshambuliaji huyu na klabu chake umezuka kutokana na swala la mishahara.
Mtana shari wake Real Madrid, Christiano Ronaldo, alisaini mkataba mpya wenye dhamani ya Euro milioni 17 kila mwaka kulingana na gazetu la Marca kumfanya awe mchezaji kabumbu anayelipwa kiasi kikubwa nchini hiyo.
Jarida la Forbes linashikilia Messi anatia kibindoni Euro milioni 16 kila mwaka kwa ulinganishi.