REAL MADRID WATAMBAA HADI 16 BORA KOMBE LA MFALME
KLABU
ya Real Madrid imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la Mfalme
Hispania baada ya kuifunga Olimpic Xativa mabao 2-0 Uwanja wa Bernabeu.
Kikosi
cha Carlo Ancelotti walijiweka kwenye nafasi ngumu awali baada ya awali
kutoa sare ya bila kufungana na timu hiyo ya Daraja la Kwanza.
Lakini
mabeki wa Real wakafanya kazi nzuri ya kutoruhusu mabao jana, huku
Asier Illarramendi akiifungia timu hiyo bao la kwanza dakika ya 16 kabla
ya Angel Di Maria kufunga la pili dakika ya 28 kwa penalti. Real sasa
itakutana na Osasuna.