SUAREZ AFURAHIA KUIWEKA LIVERPOOL KILELENI.
Luis Suarez alisherehekea mkataba wake mpya kwa kuiweka Liverpool kileleni Ligi ya Premia kwa kufunga mabao mawili na kutamba uwanjani wakati wa ushindi wa 3-1 Jumamosi dhidi ya klabu ya Cardiff City inayokabiliwa na mzozo.
Manchester City walisonga hadi nambari mbili licha ya bao la kujifunga la Vincent Kompany wakati wa ushindi wa 4-2 dhidi ya wanyonge Fulham nao mabingwa Manchester United, walio nambari saba, wakacharaza West Ham United 3-1 kupitia magoli ya Danny Welbeck, Adnan Januzaj na Ashley Young.
Suarez ambaye kwa sasa hashikiki, na aliyekuwa ameonekana kama ataondoka Anfield kipindi cha kuhama wachezaji kilichopita baada ya kupigwa marufuku kwa kumuuma mchezaji mwingine, alifunga bao la kwanza kwa ustadi mkali kasha akamwandalia Raheem Sterling la pili baada ya kupokea mpira mzuri kutoka kwa Jordan Henderson ambaye sasa ameamka.
Muda mfupi baadaye, mambo yalikuwa 3-0 baada ya Suarez kufunga bao lake la 19 ligini msimu huu kipindi cha kwanza kikiisha. Alilifunga kwa kupinda kombora kutoka nje tu ya eneo la hatari baada ya kupewa mpira wa kisigino na Henderson.
Liverpool walirarua Tottenham Hotspur 5-0 ugenini wikendi iliyopita na wangepata mabao mengi dhidi ya Cardiff kwani Suarez nusura afunge lake la tatu lakini akapokonywa na mlingoti wa goli.
"Nina furaha kutokana na mkataba mpya lakini macho yangu yote yalikuwa kwenye mechi. Tulicheza vyema kipindi cha kwanza,” straika huyo wa Uruguay aliambia kituo cha televisheni cha BT Sport.
"Ni mapema kusema (kwamba tunaweza kushinda ligi). Ni muhimu kwetu kuendelea kuangazia mechi inayofuata. Tunapocheza nyumbani, tumekuwa imara.”
Ushindi huo dhidi ya Cardiff ambao wamo nambari sita kutoka mwisho, na meneja wao aliye matatani Malky Mackay, uliwapeleka Liverpool alama moja juu kwenye jedwali wakiwa na alama 36 utoka kwa mechi 17.
Arsenal (alama 35), ambao wako nambari tatu, wanaweza kutwaa tena nambari ya kwanza wakishinda nyumbani dhidi ya Chelsea (33) walio nambari nne Jumatatu (2000 GMT).