WENGER AICHEKELEA CARDIFF ISIYO NA KOCHA.

Arsenal wana nafasi ya kuimarisha uongozi wao wa Ligi ya Premier ya Uingereza ikiwa watawachakaza Cardiff City, ambao hawana meneja, kwa mara ya pili katika kipindi kichache wakati shindano hilo litakapo rejea siku ya kuadhimisha Mwaka Mpya.

Ligi ya Premier iko katika pilika pilika za mechi ya nne ndani ya siku kumi wakati ambao wachezaji na vilabu vya nchi zingine barani Uropa viko kwenye mapumziko ya sherehe za Krismasi.

Huku ligi hiyo ikiwa imefikia kati musimu huu baada ya raundi 19 kusakatwa, Arsenal wanamiliki uongozi na alama 42, ikiwa ni mara ya kwanza kilabu hicho kuanza mwaka kileleni tangu kampeni ya 2007-08.


Manchester City (41), Chelsea (40) na Everton (37) wanawaandama katika nafasi nne bora.

Kinyang’anyiro cha mwaka huu kimechacha moto kwani Liverpool walioongoza Krismasi wameshuka ngazi hadi nafasi ya 5 na pointi 36 baada ya kupoteza dhidi ya City na Chelsea.

Vijana hao wa Brendan Rodgers ambao wataalika Hull City wamo alama mbili mbele ya mabingwa Manchester United na Tottenham Hotspur ambao watagaragazana uga wa Old Trafford Jumatano.

Katika nafasi za mwisho, pointi saba pekee zimetofautisha Swansea (21) katika nafasi ya 11 na Sunderland wanaovuta mkia.

Kwenye barua yake kwa mashabiki ya kila wiki, meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amenena kwamba kuna “kitu specheli” na kikosi chake cha sasa huku akisifu weledi wao wa kimawazo, “hili jambo limezua maswali mara mengi hapo awali.”

“Tulithihirisha hilo ugenini West Ham pale tulijiinua kutoka kufungwa 1-0 na kushinda 3-1 na turirudia tena Newcastle pale tulipofanikiwa kushinda 1-0 ingawa tulijipata hayawani katika dakika 15 za mwisho.”

“Kuna umoja na roho juu sana kikosini.”

Wenger anazungumuza na uzoefu kwani Arsenal ni miongoni mwa timu tatu zilizoongoza Mwaka Mpya lakini wakakosa kutia taji kibindoni katika mwongo mmoja uliopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA