CHELSEA WAMEKOSA MAKALI YA KUUA- MOURINHO
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alilazimika kurudia tena hadithi yake ya kawaida huku akiomboleza kushindwa kwa timu yake kufunga baada ya kubanduliwa kwa kulazwa 2-1 muda wa ziada na Sunderland katika League Cup Jumanne.
"Kiwango cha uchezaji soka ambacho tulionyesha ni kizuri sana. Hatushindwi kwenye mechi kwa sababu eti hatuchezi au kwamba mpinzani anatuzidi, ni kutokana na hali kwamba hatuui wapinzani wetu na tunawapa uhai,” Mourinho aliambia Sky Sports baada ya timu yake kubanduliwa katika robofainali.
“Kila mpinzani anajua kwamba anaweza kutufunga bao. Tulipata nafasi nyingi nzuri za kufunga na hatukufunga.”
Ingawa Chelsea wako nambari tatu kwenye Ligi ya Premia na wako awamu ya muondoano katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, matokeo ya kushangaza majuzi yamefanya Mourinho kutahadhari zaidi kuhusu uwezekano wa timu yake kushinda mataji.
Kushindwa mara mbili na kutoka sare katika mechi saba za Ligi ya Premia pamoja na kushindwa mara mbili za Basle ya Uswizi, nyumbani na ugenini Ulaya, kumewafanya wengi kuangazia mastraika butu Fernando Torres, Demba Ba na Samuel Eto'o.
Watatu hao wamefunga mabao matano pekee kwa jumla msimu wote.
Eto'o ambaye alikabidhiwa jukumu la kuongoza mashambulizi dhidi ya Sunderland alipoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la pili kipindi cha pili baada ya kuachwa yeye na kipa pekee.
Alipoulizwa ni kwa nini timu yake ya sasa Chelsea haikosi huruma kama ile aliyokuwa nayo kipindi cha kwanza alipokuwa kwenye klabu hiyo, Mourinho alisema: "Siwezi kujibu swali hili.
Mimi ni meneja wa timu hii na si ile ya awali. Hatuko nyuma ya timu hiyo ya awali, lakini tuko mbele ukiangalia kiwango.
“Lakini soka ni kuhusu matokeo na kufunga mabao. Kulikuwa na nafasi nyingi nzuri na si moja pekee. Tulitaka sana kuendelea katika dimba hili lakini hatukulipa kipaumbele. Lazima tufunge mabao na kushinda mechi sio tu kuwa timu bora kila mechi.”
Chelsea wana mechi ngumu kipindi hiki cha sikukuu, kwani watatembelea viongozi wa ligi Arsenal Jumatatu kabla ya kuwa wenyeji wa Swansea City na Liverpool.