HAKUNA KAMA CRISTIANO RONALDO TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA.

Kwa nini asiwe bora duniani? Bao alilofunga jana katika ushindi wa 2-0 dhidi ya FC Copenhagen limemfanya Cristiano Ronaldo awe mchezaji wa kwanza kufunga mabao tisa katika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mreno huyo alirejea uwanjani baada ya kukosa mechi iliyopita ya makundi ya Real Madrid dhidi ya Galatasaray na kufunga dakika ya 58. Sasa amefikisha mabao 59 katika mechi 96 kwenye michuano hiyo, akiwa amefunga katika kila mechi kati ya tano alizocheza msimu huu.

Jana angeweza kupiga Hat-trick kama asingegongesha mwamba na kukosa penalti mwishoni kipindi cha pili.

Wazi hizi ni dalili nzuri kwa Ronaldo kuelekea kilele cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Januari mwakani, akiwa ameingia fainali na Muargentina Lionel Messi wa Barcelona na Mfaransa Frank Riberry wa Bayern Munich.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA