STARS KUMKOSA ULIMWENGU DHIDI YA ZAMBIA LEO, SURE BOY AREJEA KIKOSINI

MSHAMBULIAJI tegemeo wa Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Thomas Ulimwengu atakosekana kwenye kikosi cha leo wakati timu hiyo ikimenyana na Zambia katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge 2013 Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.

Uli amesema jana kwamba anasumbuliwa na maumivu ya nyama na hali ni mbaya kiasi kwamba hawezi kucheza leo.

Uli alicheza vizuri mechi zote, za Robo Fainali Stars ikiitoa Uganda ‘The Cranes’ kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 na Nusu Fainali wakifungwa 1-0 na Kenya.

Kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyekosa mechi dhidi ya Kenya kutokana na kuwa anatumikia kadi nyekundu aliyopewa dhidi ya Uganda, leo anatarajiwa kurejea kikosini.

Mchezo huo wa mshindi wa tatu, utafuatiwa na Fainali kati ya Sudan ‘Mwewe wa Jangwani’ dhidi ya wenyeji, Kenya ‘Harambee Stars’ jioni, Uwanja huo huo wa Nyayo.


Awali kabisa, wakongwe waliowahi kung’ara na Kenya enzi hizo ‘Wazee wa Kazi’ watamenyana na wazee wenzao wa Tanzania ‘All Stars’ Uwanja wa City, kuanzia Saa 7:00 mchana.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA