BRANDTS AKACHA MAZOEZI YANGA.
Kocha wa Yanga, Mdachi Ernie Brandts amelazimika kukatisha ratiba ya mazoezi ya kikosi chake kwenye Uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama, Dar es Salaam baada ya kubaini wachezaji wake wanasumbuliwa na uchovu wa mazoezi magumu ya juzi.
Juzi Timu ya Yanga ilifaya mazoezi kwa takriban saa tatu kwenye uwanja huo huku kukiwa na kali kujiandaa kwa mchezo wa 'Nani Mtani Jembe' dhidi ya watani wao wa jadi, Simba utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Desemba 21, mwaka huu.
Lakini, Kikosi cha Yanga jana kilifanya mazoezi kwa dakika 90 tu kwenye huo tofauti na ilivyozoeleka 'Wanajangwani' kujifua kwa saa mbili.
Akizungumza baada ya mazoezi uwanjani hapo, Brandts alisema amelazimika kuwapumzisha wachezaji wake kwa vile 'hawako sawa kuendelea na mazoezi'.
"Jana (juzi) tulifanya mazoezi magumu na kwa kipindi kirefu, wachezaji hawako vizuri na wanaonekana kuwa na uchovu. Nimelazimika kukatisha mazoezi ili wapate muda wa kupumzika na kukusanya nguvu," alisema beki huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uholanzi.
Yanga iko kambi kwa wiki tatu sasa kujiandaa kwa mchezo huo na mashindano mengine yanayowakabili ikiwamo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Klabu Bingwa Afrika mwakani.