Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2024

Bodi ya Ligi yainusuru Simba kwa Tabora United

Picha
Na Ikrwm Khamees Bodi ya Ligi (TPLB) imeiondoa mechi kati ya Simba na Tabora United iliyopangwa kuchezwa Disemba 28, 2024 sasa itapangiwa baadaye. Pia mchezo dhidi ya Simba na Singida Big Stars ambao awali haukupangiwa tarehe sasa utachezwa Disemba 28, 2024 kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida. Mchezo dhidi ya Tabora United ambao ulipangwa kuchezwa Disemba 28, 2024 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora umeondolewa na utapangiwa tarehe mpya. Kusogezwa kwa mechi ya Simba na Tabora United ambayo sasa ni moto wa kuotea mbali baada ya kuzifunga Yanga na Azam na kuigomea Singida Black Stars, Bodi ya Ligi ni kama wameisaidia Simba kutoka kwenye kichapo kwa walina Asali hao wa Tabora.

KMC yaikausha Pamba jiji

Picha
KMC ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wameikausha Pamba Jiji FC ya Mwanza bao 1-0 m hezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa KMC Mwenge jijini. Bao pekee lililoipa pointi tatu muhimu limefungwa na Hance Masoud dakika ya 88, hata hivyo Pamba Jiji inayonolewa na Fred Minziro imecheza vizuri isipokuwa bahati haikuwa yao

Singida Black Stars yaipigisha kwata Prisons

Picha
Timu ya Singida Black Stars imeichapa Tanzania Prisons mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya. Mabao ya Singida Black Stars yamewekwa kimiani na Marouf Tchakei na Kennedy Juma, huo ni mwendelezo mzuri wa ushindi kwa Singida Black Stars inayonolewa na kocha wa muda Ramadhan Nswazurimo

Simba sasa ni ya tatu kombe la Shirikisho

Picha
Timu ya Bravo's de Maquis ya Angola kwasasa ndio wanaongoza kundi A kombe la Shirikisho barani Afrika huku Simba SC ya Tanzania ikishika nafasi ya tatu. Kwa mujibu wa msimamo wa kundi hilo uliopostiwa jana baada ya kumalizika kwa mechi zote, Bravo's wamekaa kileleni wakiiengua CS Constantine ya Algeria zote zikiwa na pointi 6. Lakini Simba SC ya Tanzania iliyokuwa inashika nafasi ya pili, sasa imeangukia nafasi ya tatu ingawa Ina pointi 6, CS Faxien ya Tunisia inashika mkia ikiwa haina hata pointi moja ingawa bado ina nafasi ya kwenda robo fainali.

Elie Mpanzu rasmi kuichezea Simba SC

Picha
Hatumaye kimaeeleweka kwa kiungo mshambuliaji Elie Mpanzu raia wa DR Congo kuidhinishwa katika kikosi cha Simba SC msimu huu. Mpanzu jana aliidhinishwa kwenye kikosi cha Simba na kuchukua nafasi ya kipa Ayoub Lakred, kwa maana hiyo Mpanzu ataitumikia Simba na kwenye mchezo wa keshokutwa dhidi ya KenGold huenda akavaa jezi kwa mara ya kwanza.

Prof Kabudi aishika pabaya Simba

Picha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi akemea vikali uharibifu wa viti uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Simba Sports Club ya Tanzania na CS Sfaxien ya Tunisia, Desemba 15, 2024. Prof. Kabudi amemuagiza katibu wa Wizara hiyo kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia klabu ya Simba na kuwanakili Shirikisho la mpira nchini (TFF) kwa makusudi ya kuwataka walipie gharama za uharibifu zilizofanywa katika mchezo huo wa kombe la shirikisho Afrika. Pia Prof. Kabudi ameliagiza jeshi la polisi kuwasaka wote waliohusika kwenye uharibifu huo wachukuliwe hatua za kisheria.

Bravo's yashinda, kundi sasa lishakuwa gumu

Picha
Timu ya Bravo's de Maquiz ya Angola usiku huu imelitia shaka kundi lake lenye timu za Simba SC, CS Constantine na VS Faxien baada ya kuifunga CS Constantine ya Algeria mabao 3-2 mchezo wa kombe la Shirikisho kundi B. Ushindi huo unaifanya Bravo's kufikisha pointi 6 hivyo sasa timu zote tatu kulingana pointi, Simba ya Tanzania itakuwa na kazi ngumu kwani itasafiri kuzifuata Bravo's yenye pointi 6 na CS Faxien ambayo haina pointi. Ugumu wa kundi hilo unakuja kwa Bravo's kuitaka nafasi sawa na CS Constantine nayo kuitaka nafasi, huku Simba pekee ikisaliwa na mchezo mmoja nyumbani.

Rally Bwalya mbioni kutua Pamba Jiji FC

Picha
Taarifa za kuaminika ni kuwa klabu ya Pamba Jiji FC ipo katika mchakato wa mwisho wa kupata saini ya Kiungo Rally Bwalya kutoka Napsa Stars FC Pamba Jiji FC inahitaji kuboresha kikosi chao na huu usajili wa Rally Bwalya ukiwa ni usajili wa dirisha lijalo la uhamisho Rally Bwalya aliwahi kucheza Simba SC na Power Dynamos.

Al Hilal kuhamia Libya

Picha
KWA MUJIBU Wa Micky Jnr African Football Journalist ni kwamba Klabu ya Al Hilal S.C ya Sudan Al Hilal ametuma barua kwenda CAF. Wanataka kupeleka mechi zao za nyumbani za Ligi ya Mabingwa hadi Libya. Ikiwa CAF itaidhinisha barua hii, basi watacheza kwenye Uwanja wa Benghazi.

Kibu apiga mawili, Simba ikiichapa CS Faxien

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya CS Faxien ya Tunisia mchezo wa kombe la Shirikisho uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. CS Faxien walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Hazzem Haji Hassen dakika ya 03 lakini Simba walichomoa kupitiavkwa Kibu Denis dakika ya 08. Lakini Simba waliongeza bao la pili dakika ya 98 kupitia kwa Kibu akifunga la pili na kuifanya Simba ifikishe pointi 6, timu hiyo itarudiana na Fwxien mjini Tunis, Tunisia

Gamondi kuibukia Zamalek

Picha
Klabu ya Zamalek SC ya nchini Misri inaendelea kufanya uwezekano wa kupata kocha mkuu wa klabu hio haraka sana kuendelea na mashindano ndani na nje ya nchi. Zamalek imeonyesha nia ya kumsajili aliekua kocha mkuu wa klabu ya Young Africans Sports Club Miguel Angel Gamondi. Baadhi ya majina yaliyopendekezwa na bodi ya timu ya Zamalek Sc imeorodhesha makocha watano Josef Zinnbauer Paulo Duarte Carlos Queiroz Miguel Ángel Gamondi Héctor Cúper

Dili la Kelvin Nashon kutua Yanga laota mbaya

Picha
KELVIN Nashon alikuwa katika hatua za mwisho za kujiunga na Yanga kwa mkopo akitokea Singida Black Stars ya Singida lakini kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyanzo vyangu ni kuwa dili hilo kwasasa lipo 50/50 na mbioni kuota mbawa kabisa, Yanga huenda wakajitoa dakika za mwisho kwa maana hawakamilisha uhamisho huo. Nashon (24) awali alihitajika na Pamba ya Mwanza ambapo walikubaliana maslahi na kila kitu na akasafiri mpaka Jiji la Miamba sambamba na Straika Habibu Kyombo ambapo ulikuwa ni uhamisho wa mkopo ila Kelvin alipigiwa simu baadae kuwa Yanga wanamhitaji na akasafiri kuja Dar es Salaam na walikubaliana kila kitu kabla ya kusaini kwa mkopo. Baada ya muda mchache Nashon kwa mujibu wa vyanzo vyangu hakuwa anapata tena ushirikiano kutoka kwa Yanga ili kumaliza dili hilo na hakupewa majibu ya moja kwa moja maana ilikuwa atambulishe kabla ya Israh Patrick, kuna uwezekano mkubwa Kiungo huyo akarejea Pamba aliporipiti awali kwa mkopo endapo Yanga hawatomrejea tena ndani ya siku mbili h...

Yanga warejea na bonge la rekodi

Picha
Kikosi cha timu ya Yanga SC kinewasili salama kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, (DRC) ambapo jana kilicheza na TP Mazembe na kwenda nayo sare ya 1-1 mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika. Mchezo wa jana ndio ulikuwa wa kwanza kwa Yanga kupata pointi baada ya mechi mbili mfululizo kupoteza kwa mabao mawili bila majibu. Taarifa nzuri kwa Yanga kwamba imekuwa klabu pekee hapa nchini kurudi na pointi nje ya nchi msimu huu, watani zao Simba SC waliambulia patupu nje ya nchi wakifungwa mabao 2-1 na CS Constantine ya Algeria. Mechi zilizobaki kwa Yanga zitachezwa jijini Dar es Salaam hivyo Simba pekee itatoka nje ya nchi kuzifuata timu za Tunisia na Angola ili tuone kama wataweza kuwafikia Yanga au laah.

Harmonize awashukuru mashabiki kwa kumlipia deni

Picha
Msanii Harmonize ametangaza kuwa hana deni lolote hii ni baada ya kulipa deni la milioni 10 alilokopa kutoka Benki ya CRDB. Harmonize akizungumza kupitia Instagram, ameeleza jinsi sapoti ya Mashabiki ilivyomsaidia kufanikisha hilo. Konde pia aliwashukuru CRDB kwa mchango wao katika safari yake ya muziki na, aifunga mwaka kwa kusisitiza kuwa utajiri wa kweli ni watu, si pesa

Ukata waikumba Fountain Gate, mmoja aomba kuondoka

Picha
Kama tulivyotoa taarifa kuhusu hali ya uchumi wa timu ya Fountain Gate FC ni kuwa Mchezaji Edger Williams ameomba kuondoka kwenye kikosi hicho kama asipoongezewa Mshahara! Moja wa viongozi wa timu hiyo amemuambia Ali Machius Kanyasi kuwa "Edger Williams na yeye kaomba kuongezewa Mshahara jambo ambalo anajua ni gumu kwa sasa ili asepe zake" Timu kadhaa za ligi kuu zimeanza kuangalia uwezekano wa kumchukua Mchezaji huyo! .

Yanga yaishika TP Mazembe

Picha
Mabingwa wa soka Tanzania bara Dar Young Africans jioni ya leo imeishika vibaya TP Mazembe na kuilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika uwanja wa TP Mazembe Stadium, mjini Lubumbashi, DR Congo. TP Mazembe walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Cheick Fofana dakika ya 40, Yanga walisawazisha kupitia Prince Dube dakika ya 90. Kwa matokeo hayo Yanga itaendelea kushika mkia ikiwa na pointi 1 wakati Mazembe pointi 2. .

Yanga kujinasua mkiani leo?

Picha
Wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Yanga SC, leo wanakwenda kutupa karata yao muhimu katika mchezo wa tatu wa Makundi dhidi ya TP Mazembe baada ya kupoteza michezo miwili ya kwanza. Yanga leo anahitaji ushindi kwa namna yoyote ili walau kuanza kupata mwanga wa kuamka kuelekea kwenye kufuzu kwenda Robo Fainali endapo watazichanga vizuri karata zao katika michezo mingine mitatu itakayokuwa imesalia. Msimamo kwenye kundi A la Yanga upo hivi: Al-Hilal - alama 6 MC Alger - alama 4 TP Mazembe - alama 1 Yanga alama - 0

Fountain Gate yabeba mchezaji aliyeachwa na Coastal

Picha
Baada ya klabu ya Coastal Union kutangaza kuachana na mchezaji Jackson Shija ni rasmi sasa mchezaji huyo atajiunga na timu ya Fountain Gatr ya mkoani Manyara kama mchezaji huru,awali duru zilieleza ya kwamba angejiunga na Pamba Jiji FC . Usajili wa dirisha dogo baadhi ya timu zinajiimarisha ili kuonesha ushindani na kubaki Ligi Kuu na nyingine kuwania ubingwa. Kwa vyovyote usajili wa Shija unaweza kuwa na faida kubwa kwa Fountain Gate kwakuwa ana kiwango kizuri

Aziz Ki arudisha "Pacome staili"

Picha
Hali imeanza kubadilika kwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Stephanie Aziz Ki baada ya jana kupost picha zake akionesha muonekano wa nywele zake akiwa amepaka brichi. Mchezaji huyo msimu uliopita aling' ara akiwa na brichi nyeupe ambayo alianza kuonekana nayo kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya CS Belouzdad ya Algeria. Mchezaji huyo alikuwa ananyoa kawaida lakini alidilika kwa sababu kwenye mechi hiyo Yanga iliwataka wachezaji wote kumuiga Pacome Zouzoua kwakuwa ilikuwa siku ya Pacome Day na happy ndipo alipoanza kuutumia mtindo huo

Singida Black Stars yamtema kipa wa Sierra Leone

Picha
Taarifa kutoka Singida Black Stars zinasema kuwa klabu hiyo imesitisha mkataba wa golikipa Mohamed Nbalie Kamara ambaye pia ni golikipa wa timu ya taifa ya Sierra Leone. Golikipa huyo amekuwa akisugua benchi huku langoni akisimama golikipa mzawa Metacha Mnata aliye katika kiwango bora sana tangu msimu uanze.

Ronaldo kucheza kombe la dunia la 2030

Picha
Nyota wa zamani wa Manchester United na taifa la Ureno Luis Nani amesema Cristiano Ronaldo anaweza kucheza kombe la Dunia 2030 ambalo litaandaliwa na Ureno sambamba na Uhispania na Morocco ikiwa tu atazingatia mlo maalum Ronaldo mwenye umri wa miaka 39 ataiwakilisha Selecao katika Kombe la Dunia la 2026 akiwa na miaka 41 lakini bado hajaweka wazi kuhusu kombe la dunia la 2030 ambapo atakuwa amefikisha miaka 45 licha ya mara kadhaa kukanusha malengo ya kustaafu soka hivi karibuni “Ronaldo anajituma sana na ananidhamu ya soka unaweza kuona umri umeenda lakini bado anafunga kila siku” Nani

Tabora United yaleta balaa Azam FC

Picha
Timu ya Tabora United jioni ya leo imeichapa Azam FC mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mabao yote ya Tabora United leo yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Ma Olongi Makambo moja kila kipindi akimtungua kipa namba moja wa timu ya taifa ya Sudan, Mohamed Mustafa kwa kichwa dakika ya 37 na kwa shuti la mguu wa kushoto 68.

Ramovic anataka wachezaji watano wapya Yanga

Picha
TAARIFA zandani zinaeleza kuwa kocha SEAD RAMOVIC amewaambia viongozi anataka wachezaji wasiopungua watano kwenye dirisha dogo linaloanza Jumapili ijayo. . Kocha anataka kipa ambaye haachani mbali kwa ubora na Djigui Diarra, beki wa kushoto, beki wa kati, kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji anayeliona goli.

Fountain Gate mwendo mdundo yailaza Coastal Union

Picha
Timu ya Fountain Gate jioni ya leo imeifunga Coastal Union mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa Tanzanite mjini Manyara. Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Elie Mukoko dakika ya 15, William Edgar dakika ya 48 na Nickolas Gyan dakika ya 56, wakati mabao ya Coastal Union yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya 44 na Maabad Maulid dakika ya 80

KWANINI YANGA WANAPENDA KUSAJILI WACHEZAJI WA SIMBA?

Picha
Na Prince Hoza ISRAEL Patrick Mwenda nj miongoni mwa wachezaji wapya wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, mchezaji huyo alisajiliwa wiki hi akitokea Singida Black Stars ya mkoani Singida. Mwenda ana uwezo wa kucheza namba mbili au tatu na alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Simba SC aliyojiunga nayo akitokea KMC. Usajili wa Mwenda umepokelewa kwa mitizamo tofauti, huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakigawana makundi, wapo wengine wanaupongeza uongozi wa Yanga kwa kumsajili wakiamini kwamba Mwenda anaweza. Lakini pia kuna wengine wanatilia shaka usajili wake wakisema hafai na anauwezo wa kuitumikia Yanga kwa sababu alikuwa hapati namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba. Kusajiliwa kwake Yanga si sahihi kwani ana uwezo wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza, tayari Yanga ina mabeki wa pembeni na wenye uwezo mkubwa na sidhani kama Mwenda ataweza kupata nafasi ya kucheza. Yanga ina mabeki kama Kouassi Attoholoa Yao Jeshi na Chadrack Boka ambao wamek...

KMC, Mashujaa zatoka suluhu

Picha
WENYEJI, KMC wametoka suluhu na Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Ushindani umeonekana kuwa mgumu kwenye ligi hiyo.

Yanga yakimbilia kwa Mungu

Picha
#MICHEZO: Rais wa klabu wa Yanga Hersi Said amesema anajua umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe mchezo utakaochezwa jumamosi hii, disemba 14, 2024. "Tumuombe Mungu twende salama tukaipiganie timu yetu najua ni muhimu kupata matokeo katika mchezo huu, viongozi wanakwenda pamoja na wachezaji, benchi la ufundi ili kuipigania timu yetu na kutafuta matokeo, ikimpendeza Mungu basi turudi na alama tatu."- Eng. Hersi Rais Yanga SC. Ilikujiweka kwenye eneo salama Yanga wanahitaji ushindi kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe Utakaochezwa Lubumbashi nchini Kongo (DRC) hadi sasa Yanga wapo mkiani kwenye msimami wa kundi A’, hawana alama hata moja baada ya kufungwa michezo yote miwili waliyocheza. Al Hilal ndio kinara wa kundi alama 6, Mc Alger nafasi ya pili wana alama 4 na Mazembe wana alama 1 nafasi ya tatu.

Singida Black Stars yaichapa Dodoma Jiji

Picha
Timu ya Singida Black Stars leo imefufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi Kuu bara baada ya kuilaza Dodoma Jiji mabao 2-1. Mabao yote ya Singida Black Stars yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Elvis Baranga Rupia dakika ya nane na 15, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefungwa na mshambuliaji mzawa, Yasin Mohamedi Mgaza 58.

Elie Mpanzu kuwavaa KenGold

Picha
Winga mpya wa Simba SC Elie Mpanzu Kibisawala sasa ni rasmi ataanza kutumika kwenye mechi dhidi ya KenGold itayopigwa siku ya tarehe 18 mwezi huu Dirisha la usajili la ndani linafunguliwa tarehe 16 mwezi huu na kufungwa tarehe 15 Januari na la CAF litafunguliwa tarehe 1 mwezi Januari na kufungwa tarehe 31 Januari hivyo upande wa kombe la Shirikisho Mpanzu ataanza kutumika kuanzia mechi na CS Faxien itayochezwa nchini Tunisia

Simba yamzuia Lawi kwenda Yanga

Picha
BAADA ya tetesi kuibuka Yanga wanamhitaji beki wa Coastal Union Lameck Lawi,mabosi wa Simba wameamua kuifufua upya kesi dhidi ya mchezaji huyo TFF. Kitendo cha beki huyo kuhusishwa na Yanga kimewaamsha upya mabosi wa Msimbazi na kuamua kukimbilia TFF kuifufua kesi hiyo ambayo taarifa zinaeleza kuwa kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa leo Alhamisi.

Baleke atemwa, ahusishwa Namungo

Picha
Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga,Jean Baleke atawakosa waajiri wake kuelekea kwenye mechi ya kimataifa ya michuano ya klabu bingwa barani Africa ya CAF. Baleke hajasafiri na kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa klabu bingwa barani Africa ambapo Yanga SC watacheza na TP Mazembe ya nchini DR Congo. Wakati huo huo mshambuliaji huyo anahusishwa kujiunga na timu ya Namungo FC ya Ruangwa na tayari wameanza mazungumzo kabla ya kusajiliwa katika dirisha hili dogo la Januari

Malengo yetu ni kufika robo fainali- Fadlu

Picha
Kocha mkuu wa Simba SC Fadlu Davids amesema malengo yao kama timu ni kufuzu hatua ya robo fainali kama vinara wa kundi A kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani afrika msimu huu 2024-25. “Kundi bado lipo wazi tunapaswa kupambana kuiwania nafasi ya kwanza kwenye kundi. Kufuzu robo fainali ndio lengo namba moja, lakini kama ukifuzu kama kinara wa kundi utakuwa na faida hatua ya robo fainali.’’ - Fadlu Davis kocha Simba SC Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A ikiwa na alama 3 katika michezo miwili waliyocheza mpaka sasa. Wameshinda mchezo mmoja pia wamefungwa mchezo mmoja tofauti yao na kinara wa kundi CS Constantinois ni alama 3.

Cedric Kaze kurejea Jangwani

Picha
Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga SC Cedric Kaze raia wa Burundi anarejea ndani ya klabu hiyo. Kaze anarejea kikosini humo kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Saed Ramovic, Muda wowote kuanzia sasa kocha Kaze atawaaga wachezaji wa klabu yake ya sasa ya Kaizer Chiefs na kuanza safari ya kuja Tanzania kuanza majukumu yake mapya ndani ya waajiri wake wa zamani Young Africans.

Aucho arejea mazoezini Yanga

Picha
Kiungo wa Yanga raia wa Uganda Khalid Aucho amerejea mazoezini huku akionekana kuwa fiti na kuimarika zaidi tayari kuitumikia Yanga kwenye mchezo wa jumamosi dhidi ya Mazembe Huku kwa upande wa Clement Mzize naye akirejea mazoezini ingawa taarifa zinaeleza kuwa hatokuwa tayari kutumika katika mchezo wa jumamosi dhidi ya Mazembe kwa dakika zote , tofauti na Aucho anayeonekana kuwa tayari zaidi!!

Pamba Jiji yaibana JKT Tanzania

Picha
WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya bila mabao na Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.  Hii ni dalili nzuri kwa Pamba Jiji inayonolewa na Fred Minziro ambaye tangu alipoichukua timu hiyo imekuwa na mwenendo mzuri.

Micky Harvey Ossété kumrithi Aucho Yanga

Picha
Anaitwa Micky Harvey Ossété,Raia wa Congo-Brazzavile huyu ni kiungo Mkabaji tegemezi katika kikosi cha Saint Eloi Lupopo ya Kinshasa Congo. Huyu mwamba anakaba mpaka Mawimbi ya sauti za Mashabiki, anajua pia kufunga na kuanziasha Mashambulizi,ndiyo kiungo Shoka pale Congo Brazzaville. Katika michuano yote ya kimataifa yaliyohusisha timu za Taifa kwa asilimia zaidi ya 85 ametumikakatika kikosi cha timu ya Taifa ya Congo Brazzaville ,pia Saint Eloi Lupopo imemtumia sana katika kusaka tiketi ya kufuzu hatua za Makundi CAF Confederation Cup ✨ Hata hivyo vilabu kadhaa Africa kusini vipo kwenye vita Kali kupata Saini yake ikiwa Yanga Watampata huyu mwamba basi tatizo la Mawasiliano na miundombinu uwanjani basi litakuwa limetibika Ossété yupo tayari kujiunga na Yanga ,japo kwa upande yanga bado halijawekwa wazi. Kama uhamisho wake ukikamilika basi defensive Midfielders watakuwa hawa. 1.Kelvin Nashon 2.Khalid Aucho 3.Micky Harvey Ossété 4.jonas mkude 5.Aziz Andambwile

KenGold yanasa kifaa Murmbe Makumbi City

Picha
Klabu ya Ken Gold inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara iko mbioni kukamlisha usajili wa kiungo fundi wa Muembe Makumbi City Nasir Ali Abdalla Nassir Bofu. Bofu anatarajiwa kucheza mchezo wake wa mwisho kwenye kikosi Cha Muembe Makumbi City dhidi ya JKU Disemba 14.

Yanga kuachana na Andambwile

Picha
Klabu ya Yanga SC imefanya mazungumzo na Kiungo Aziz Andabwile ili kufikia makubaliano ya kuachana nae katika dirisha dogo la uhamisho Kiungo Aziz Andabwile anatajwa kupisha usajili mpya wa Yanga SC katika maboresho ya klabu hiyo Aziz Andabwile aliwahi kucheza katika klabu ya Mbeya City FC kabla hajajiunga na Singida Big Stars.

Israel Mwenda atambulishwa Yanga SC

Picha
Klabu ya Yanga SC imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa pembani Israel Mwenda kutoka Singida Black Star kwa mkopo wa miezi sita wenye kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja akifanya vizuri. Taarifa za kusajiliwa Mwenda kwenye kikosi hicho zilianza kuvuja tangu mwanzoni mwa msimu wakati anaichezea Simba SC kabla ya kuvunja mkataba. Mwenda aliyeibukia Aliance ya jijini Mwanza, ana uzoefu mkubwa wa kucheza mashindano ya kimataifa hivyo Yanga wamepata mtu sahihi, pia anaweza kucheza nafasi zote za prmbeni na anajua kupiga free kick.

Maimuna Kaimu aing' arisha Zed FC, Misri

Picha
Nyota wa Tanzania Maimuna Kaimu akiwa na timu yake ya Zed FC leo wamepata ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Pyramids FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Misri. Ushindi ambao umeifanya timu hiyo kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo

Vibonde Yanga kuwafuata Mazembe kesho

Picha
Kikosi cha Yanga Sc kinatarajiwa kuondoka kesho nchini saa 5 Asubuhj kuelekea Lubumbashi , DR. Congo kwa ajili ya mchezo wa tatu wa makundi ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe. TP Mazembe dhidi Yanga SC mchezo wao utapigwa Desemba 14, Stade TP Mazembe . Yanga na Mazembe matokeo yao si mazuri kwani Yanga haina pointi hata moja wakati Mazembe Ina pointi moja huku zote zimecheza mechi mbili

Mshahara mpya wambakisha Feitoto, Azam FC

Picha
Kiungo Feisal Salum amekubali ofa ya USD 12,000 (Tshs 31.5m) ambao ni mshahara kutoka Azam FC ili kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na USD 320,000 (Tshs Milioni 841.8) ambao ni ada ya usajili Hakuna nafasi ya Feitoto kujiunga na Simba SC katika dirisha hili dogo la usajili na ataendelea kuitumikia Azam FC katika kipindi hiki baada ya Menejiment kukubali ofa hiyo. Feitoto amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na nusu katika klabu ya Azam FC.

Simba Queens na JKT Queens hakuna mbabe

Picha
Timu ya Simba Queens imelazimkshwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya JKT Queens kwenye uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya wanawake Tanzania bara. JKT Queens walitangulia kupata bao kupitia Elizabeth Wambui na Simba Queens walisawazisha kupitia kwa Donisia Minja.

Msimchukulie poa Israel Mwenda- Geoff Lea

Picha
Mchambuzi wa soka kutoka kituo cha Crown FM Geoff Lea amesema kwamba beki wa kulia Israel Mwenda anayejiunga na Yanga kutokea Singida Black Stars ni mchezaji mzuri na watu wasimchukulie poa. "Watu wanamchukulia Israh poa, ila wakati yupo Alliance alikuwa mshambuliaji halafu kingine watu wasichokifahamu kuhusu Israh ni mpiga free kicks mzuri tu. "Kuna 'mahusiano mazuri kati ya Yanga na Singida Black Stars , Kevin Nashon, Israh, Guede, Mauya, Kibabage, hawa wote wametoka Yanga Sc kwenda Singida Black Stars na Singida kwenda Yanga Sc" Amesema Geoff Lea mchambuzi wa Crown FM Israel Mwenda

Simba ni nzuri kuliko Yanga- Ahmed Ally

Picha
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema timu yao ni nzuri kuliko ypyote katika ukanda huu wa Afrika mashariki, ina maana Simba ni nzuri kuliko Yanga. "Timu yetu ni bora kuliko timu nyingine yoyote kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, timu yetu imeimarika sana Mwanasimba inabidi ujivunie timu yako maana ubora wa kikosi unaongezeka siku hadi siku Mchezo wa Jumapili lazima kila Mwanasimba ajue umuhimu wake maana mpinzani tunayekutana nae anataka kufufukia kwetu na sisi hatuko tayari kuona CS Sfaxien anafufukia kwetu Hakuna ambaye amewahi kupata uhai ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa." Semaji Ahmed Ally

Kenya yapokwa uenyeji CHAN

Picha
Shirikisho Soka barani Afrika CAF limetoa taarifa kuwa taifa la Kenya limeshindwa kukidhi vigezo vya kuwa mmoja wa mataifa yatakayoandaa mashindano ya CHAN mwakani 2025 mara baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo. Viwanja vyote vilivyopo Kenya havina ubora wa kutumika katika michezo ya FIFA Wala CAF Kwa mujibu wa wakaguzi wa CAF na hata uwanja wa Kasarani unaojengwa pia imeonekana kuwa hautakamilika Kwa wakati. Naafasi hiyo wamepatiwa Rwanda mara baada ya kuonekana wao wamekidhi vigezo vya kuwa wenyeji wa CHAN. CHAN 2025 itachezwa katika mataifa matatu ambayo ni Rwanda Tanzania pamoja na Uganda