Simba yaitambia Singida Black Stars nyumbani kwao
Timu ya Simba SC maarufu Wekundu wa Msimbazi, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye uwanja wa Liti mjini Singida mchezo wa Ligi Kuu bara.
Kwa ushindi huo sasa Simba imefikisha pointi 40 na mechi 15 na kukaa kileleni huku ligi ikienda kusimama kupisha brecking, bao pekee la Simba limefungwa na Fabrice Ngoma dakika ya 42.
Kesho watani zao Yanga SC watawaalika Fountain Gate katika uwanja wa KMC Complex Mwenge jijini Dar es Salaam, Yanga hata kama ikiehinda haitaweza kuifikia Simba.