Nabi akalia kuti kavu Kaizer Chief
Kocha wa Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi, aliyewahi kuinoa Yanga kwa mafanikio makubwa.
Nabi anakabiliwa na shinikizo kubwa la kurejesha heshima ya timu hiyo, kwani ikiwa nafasi ya tisa kwenye ligi ya Afrika Kusini inaashiria huu ni msimu mwingine uliojaa matokeo yasiyoridhisha.
Mashabiki wa Amakhosi wanaanza kutilia shaka kama Nabi ndiye mtu sahihi wa kushindana na mahasimu wao, Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns.