Kushuka kiwango kumemuondoa Namungo, Djuma Shabani
BAADA ya kuitumikia Namungo kwa muda wa miezi sita kabla ya kutangazwa kutemwa, beki wa zamani wa AS Vita na Yanga, Djuma Shaban amefunguka sababu za kuvunja mkataba na Wauaji wa Kusini hao akisema ni kushindwa kutumika mara kwa mara kikosini.
“Tangu nimejiunga na Namungo sina mwendelezo mzuri wa kucheza, hiyo haikuwa afya kwangu na kwa timu kwa vile walinisajili ili nicheze, naamini katika upambanaji na kucheza,”
“Nimeamua kujipumzisha kwa muda ili kujiweka kwenye utimamu mzuri nitarudi tena kucheza nikiwa imara na nitacheza kwa mafanikio.”
“Nimecheza misimu miwili nikiwa na Yanga sasa nimemalizana na Namungo kuna utofauti mkubwa nimeuona, kuna mabadiliko ya timu na timu pia kuongezeka kwa wachezaji wa kigeni kwa timu tofauti,” - Amesema Djuma Shaban