Kocha wa makipa Geita Gold afungiwa kisa kushika nyeti za mwamuzi
Kocha wa Makipa wa Geita Gold, Augustino Malindi, amefungiwa mechi 16 pamoja na faini ya Milioni 1 kwa kosa la kumshika sehemu za siri mwamuzi wa akiba katika mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Geita Gold.
Baada ya kuonywa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi namba moja (1) wa mchezo huo.
Kocha huyo alitenda kosa lingine akiwa anakwenda vyumbani baada ya kuonywa kwa kadi nyekundu, kwa kumshika kifuani mratibu wa mchezo huo ambaye ni mwanamke jambo ambalo ni kinyume na maadili ya ukocha na mpira wa miguu kwa ujumla. Pia amefungiwa mechi 3 na faini 500,000 kwa kumtukana Ass Ref 1.