Opah Clement naye asajiliwa Saudi Arabia
Kapteni wa timu ya taifa ya Tanzania, Twiga Stars, Opah Clement, amejiunga na klabu ya AlUla FC Women inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia.
Opah amejiunga na AlUla akitokea SD Eibar ya Ligi Kuu nchini Hispania ambayo ameitumikia kwa msimu mmoja, huku klabu hiyo ya Alula ikiwa tayari imemtambulisha rasmi kama mchezaji wake mpya.
