Libasse Gueye ashinda tuzo ya mwezi NBC Primier League

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia Kamati ya Tuzo za TFF imemtangaza kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya NBC (2026/27), huku kocha mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi, akitwaa tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi huo.

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora na kutoa mchango mkubwa katika michezo mitano ambayo Simba ilishinda yote.

Akifunga bao moja na kuhusika kwenye mabao mengine matano (Assist 5) hivyo amehusika kwenye Magoli 6, Amewashinda Maxi Nzengeli (Young Africans) na Oscar Mwajanga (Mbeya City) walioingia naye fainali.

Kocha wa Young Africans, Manqoba Mngqithi, amechaguliwa kuwa kocha bora baada ya kuiongoza timu yake kushinda michezo yote mitano na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Amewabwaga Steve Barker (Simba SC) na Florent Ibenge (Azam FC).


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI