Harmonize aenda kumpa pole Samia Kizimkazi
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Rajab Abdul Kahali 'Harmonize' amefika kumpa pole na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 11, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Maalim Hafidh amefariki dunia Septemba 7, 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.
