TP Mazembe hiyoo raundi ya kwanza
Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya kuiondosha Medeama SC ya Ghana kwa matokeo ya jumla ya 4-1 kwenye hatua ya awali.
TP Mazembe imechomoza na ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa Lubumbashi baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa huko Ghana wiki iliyopita.
FT: TP Mazembe π¨π© 3-1 π¬π Medeama SC
⚽ 03' Mwaungulu
⚽ 19' Kazema
⚽ 88' Mwaungulu
⚽ 90+2' Amponsah
TIMU ZINGINE ZILIZOFUZU HATUA YA PILI:
πΏπ¦ Orlando Pirates
πΈπ© Al Merreikh SC
πΈπ© Al Hilal Omdurman
πΈπΈ Al Merreikh Bentiu FC
πΏπΌ Scottland FC
π²π¬ CFFA FC
π²π¦ Maghreb Fez FC
π¦π΄ Petro de Luanda
π³π¦ African Stars
