CFFA FC mpinzani wa Yanga ajae
Baada ya Young Africans kufuzu kwa kuitoa Gaborone United ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-2, sasa Yanga imepata mpinzani mwingine kutoka ukanda wa Afrika ya Kusini katika hatua ya pili ya mchujo wa CAF Champions League 2026/27.
Yanga itakutana na CFFA ya Madagascar, ambayo imefuzu baada ya kuiondoa Lijabatho FC ya Lesotho kwa jumla ya mabao 3-1.
CFFA ilishinda 2-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani, kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini kwenye mchezo wa marudiano, na hivyo kusonga mbele kwa jula ya 3-1.
Mchezo wa kwanza: CFFA vs Yanga
Oktoba 16–18, 2026
Mchezo wa marudiano: Yanga vs CFFA
Oktoba 23–25, 2026
Yanga itaanza kibarua hicho kwa kusafiri hadi Madagascar, kabla ya kurejea Tanzania kwa mchezo wa marudiano ambapo itatafuta tiketi ya kusonga mbele katika mashindano hayo.
