Eto'o atuhumiwa kulamba bilioni 1.7

Samuel Eto’o yuko kikaangoni baada ya kupewa tuhuma za matumizi ya pesa hovyo. kwa taarifa kutoka vyanzo vya habari, vinaeleza kuwa nyota wa Barcelona, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT),

Kuna kiasi cha pesa fulani hakionekani, na kiwango hicho si chini ya takribani dola 665,000 [TZS bilioni 1.7], zilizohusishwa na malipo ya mchezo wa kirafiki kati ya Cameroon na Urusi mwaka 2023.

Kufuatia sakata hilo, Eto’o, ambaye amekuwa akiongoza FECAFOOT tangu mwaka 2021, wataanza zoezi la uchunguzi dhidi ya jambo hilo linalomkabili.

Kwa upande wa mshitakiwa ambaye ni Eto’o, amesema kuwa upande wake uko wazi kwa uchunguzi zaidi ili kuona wapi amekosea. Pia, nyaraka zake zote zitaanza kuchunguzwa, na kuripotiwa kuonyesha kuwa fedha hizo ziliagizwa kutumwa kwenye akaunti yake binafsi katika benki nchini Qatar.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI