Singida BS yafanya balaa kombe la Shirikisho
Timu ya Singida Black Stars ya Tanzania imetinga raundi ya kwanza kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuilaza Al Ghazala ya Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 10-1 kufuatia jioni ya leo kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kushinda 3-0.
Mabao yaliyoiwezesha timu hiyo kutinga hatua hiyo yamefungwa na Jonathan Sowah aliyefunga mawili na Henry David moja kwa matokeo hayo Singida BS inaenda kukutana na Tusker ya Kenya.
