KOCHA Mkuu wa Twiga Stars, Bakar Shime amevunja ukimya juu ya ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa timu hiyo, Clara Luvanga kutoitwa kikosini akisema anaumizwa na kitendo cha watu kulalamika ilihali yeye ndiye aliyemtengeneza nyota huyo anayecheza soka la kulipwa Saudi Arabia. . “Hakuna aliyekuwa anamjua Clara, mimi ndio nilimuibua nilipomtoa nikaamini uwezo wake na kumfundisha hadi akawa vile na kuisaidia timu kukata tiketi ya Kombe la Dunia U17 zilizopota. Mimi ndiye najua ninachohitaji katika timu ili kupata matokeo, naumia nikisikia watu wanaongelea ishu hiyo, halafu watu hawajui, mie ndiye nilimpeleka Saudia,” alisema Shime bila kufafanua kilichomfanya asimuite kwa sasa. . Clara anayekipiga Al Nassr ya Saudia inayoshiriki Ligi Kuu, hadi sasa amefunga mabao sita kwenye mechi tano akiwa ni mmoja ya nyota tegemeo wa timu hiyo, lakini jina lake halipo kwenye kikosi cha Twiga kilichoitwa juzi kuingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Afrika (WAFCON) dhidi ya Togo