TABIA BATAMWANYA ATUA RADA ZA EXTRA BONGO
Na Said Mdoe
Mwimbaji wa kike Tabia Jumbe Batamwanya amenasa kwenye rada za Extra Bongo.
Tabia anayetamba na wimbo wake "Narudi Nyumbani" atatambulishwa kama msanii wa Extra Bongo Jumamosi hii pale Andrew's Lounge, Sinza jijini Dar es Salaam.
Extra Bongo ipo kambini ikijifua na onyesho lao la uzinduzi wa bendi litakalofanyika Jumamosi hii ambapo kikosi chao chote kitawekwa hadharani.
Saluti5 imehakikishiwa kuwa Tabia Batamwanya atakuwa sehemu ya wasaniii wa Extra Bongo watakotambulishwa Jumamosi.
Hata hivyo, Batamwanya si sehemu ya wasanii waliopo kambini bali yeye atajiunga na kambi ya Extra Bongo baada ya onyesho la Jumamosi.
Kusajiliwa kwa Tabia Batamwanya, kunafanya Extra Bongo iwe na waimbaji wawili wa kike.