CHE MALONE AWAANGUKIA MASHABIKI SIMBA
Baada ya jioni ya leo Simba kulazimishwa sare na Asec Mimosas ya Ivory Coast katika uwanja wa Mkapa jijini Dar ea Salaam ya 1-1 mchezo wa makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika, beki wa kati Che Fondoh Malone amewaangukia mashabiki wa timu hoyo.
“Tunacheza kwaajili ya Simba Sc, tunaiwakilisha Simba Sc, kwahiyo tunawaomba mashabiki watusapoti".
Mashabiki waungane na sisi na sio kututelekeza wenyewe kwani Mashabiki wetu ni familia yetu hivyo wakituacha watakuwa sio miongoni mwetu” Amesema Che Malone.