YANGA YAPIGWA FAINI YA MIL 5
Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Shilingi 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi katika mchezo wa Derby ya Kariakoo uliowakutanisha Simba na Yanga kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 5, 2023.
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia, jambo lililosababisha mchezo huo kuchelewa kuanza kwa dakika nne (4).