SIMBA YAFUNGIWA KUSAJILI
Klabu ya Simba imefungiwa kusajili mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mauzo ya mchezaji Pape Sakho.
Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mara baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya nyota huyo.