KIBU, INONGA, DIARRA WAPIGWA FAINI YA LAKI 5
Kamati ya Undeshaji na Usimamizi wa Ligi imewatoza faini ya Tsh. Laki tano (500,000) Wachezaji wa Simba SC, Kibu Denis na Henock Inonga , pamoja na golikipa wa klabu ya Yanga Djigui Diarra kwa makosa tofauti waliyoyafanya wakati wakishangilia magoli yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC kati ya Simba dhidi ya Yanga SC.
Kibu Denis ametozwa faini hiyo kwa kosa la kushangilia bao lake mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga huku akionyesha ishara ya kuwafunga midomo wakati Inonga yeye ametozwa faini hiyo kwa kosa la kushangilia bao mbele ya Maafisa wa Benchi la Ufundi la Yanga SC.
Pia kwa upande wa golikipa wa Yanga Djigui Diarra ametozwa faini hiyo kwa kosa la kwenda kushangilia mbele ya benchi la ufundi la klabu ya Simba mara baada ya timu yake kufunga moja ya mabao katika mchezo huo wa Kariakoo Derby.