DOGO ANAYECHEZA AUSTRALIA AIZAMISHA NIGER KOMBE LA DUNIA
Na Mwandishi Wetu
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku wa leo imeanza vema kampeni yake ya kufuzu fainali za kombe la dunia baada ya kuilaza Niger bao 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika mjini Marrakesh nchini Mprocco.
Bao pekee lililoifanya Taifa Stars ichomoze na ushindi limefungwa na mchezaji wake Charles M' mombwa anayecheza soka la kulipwa Australia.
Stars itarejea mapema kesho kujiandaa na kukutana na Morocco mechi ambayo itafanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Novemba 21 mwaka huu