AYOUB LAKRED KICHEKO UJIO WA BENCHIKHA SIMBA
Ayoub Lakred ni moja ya wachezaji wenye furaha zaidi katika kikosi cha @simbasctanzania baada ya ujio wa kocha mpya Abdelhak Benchika .
Golikipa huyu mtoa michomo leo ameonekana akifanya mazoezi kwa juhudi kubwa huku akiwa na tabasamu muda wote .....Ni wazi ujio wa Benchika umemfurahisha sana Golikipa huyu .
Mwamba ataendelea kulinda lango la Simba wakiwa ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy .....wakati Manula anaendelea kuuguza majeraha yake .