Coutinho arejea Yanga kuchukua nafasi ya Chirwa

Na Saida Salum, Dar es Salaam

Andrey Coutinho yupo nchini kwa lengo kuu moja tu kuja kujaribu bahati yake ya kuitumikia Yanga SC kwa mara nyingine tena. .

"Kama ukisikia nimerudi katika ligi kuu Tanzania basi jua nimerudi katika klabu nnayoipenda Yanga, siwezi kuichezea timu yoyote zaidi ya Yanga . . Nimegundua soka la Yanga linahitaji nguvu na akili, sasa nipo kamili!

"Ntasubiri hapa kwa siku 5 kuangalia uwezekano wa kujisajili Yanga, nimepanga kesho kuwepo uwanjani kuwasalimia mashabiki na wachezaji wenzangu"alimalizia raia huyo wa Brazil.

Coutinho amemaliza mkataba wake katika klabu ya Rakhine United FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Myanmar barani Asia akifanikiwa kutupia wavuni magoli 10.

Haya ya Coutinho yakiendelea winga Mtanzania Mrisho Ngassa anaendelea kusotea ombi lake mara baada ya kuomba kurudi Yanga ili amalizie soka lake kiheshima katika klabu aipendayo.

Ngassa ambaye alivunja mkataba na klabu yake ya Free State ya Afrika Kusini kwa kile kinachodaiwa kuwekwa benchi mara kwa mara na kocha Mfaransa wa timu hiyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA