Simba kusahihisha makosa kwa Ruvu Shooting leo?
Saida Salum, Dar es Salaam
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, jioni ya leo wanashuka uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuwakabili Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Simba wanataka kusahihisha makosa yao kwani katika mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu walilazimishwa sare tasa ya 0-0 hivyo leo hawatakubali kulazimishwa tena sare.
Ikiwa chini ya washambuliaji wake Laudit Mavugo raia wa Burundi, Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast na Ibrahim Ajibu 'Kadabla' kwa vyovyote wataondoka na pointi tatu.
Nao Ruvu Shooting ya Masau Bwire nayo itamtegemea zaidi kiungo wake mkongwe Shaaban Kisiga 'Marlone' ambaye aliwahi kuichezea Simba katika misimu kadhaa iliyopita