Kocha wa zamani wa Simba Afariki
Simba SC imeendelea kupatwa na misiba ya makocha wake wa zamani hasa baada ya kumpoteza kocha wake Mohamed Hassan Msomali, na jana usiku, James Agrey Siang' a amefariki dunia.
Siang’a aliidakia timu ya Taifa ya Kenya mwaka 1972 katika fainali za mataifa ya Afrika. Siang’a aliifundisha timu ya Taifa Kenya kati ya mwaka 1999 na 2000.
Baada ya hapo alikuja Tanzania akateuliwa kuifundisha Taifa Stars mwaka 2002. Siang’a alikwishapata vifundisha vilabu vya Simba SC na Moro United pia na Express ya Uganda.Octoba 2004, akiwa katika klabu ya Moro United, Siang’a aliteuliwa tena kuwa kocha wa Taifa Stars lakini alikataa wadhifa huo.
Kabla ya kuifundisha Gor Mahia ya Kenya, ikumbukwe Siang'a alitokea Mtibwa Sugar ambayo ndiyo ilikuwa klabu yake ya mwisho kuifundisha hapa Tanzania.
"Ni kweli tumempoteza ndugu yetu Siang'a. Amefariki ijumaa usiku kufuatana na taarifa tulizopewa na familia yake, tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwao ili tujue nini kinaendelea. Mungu apumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi," Oyugi raia wa Kenya akitaarifu.
Siang' a atakumbukwa sana na Wanasimba hasa baada ya kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi Ligi ya mabingwa barani Afrika na kuiondosha Zamalek ya Misri waliokuwa mabingwa watetezi