Ngasa aitosa Yanga, atimkia Oman

Na Saida Salum, Dar es Salaam

Mshambuliajj wa zamani wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Halfan Ngasa ameikacha rasmi Yanga na kuamua kutimkia nchini Oman kujiunga na klabu kongwe ya Fanja inayoshiriki Ligi kuu.

Ngasa ameondoka na ndege Alhamisi na anatazamiwa kuingia mkataba na timu hiyo, kabla hajaondoka, Ngasa alizungumza na mwandishi wa habari hizi kuwa ameshafanya mazungumzo na Fanja na wamemtumia tiketi ya ndege ili akamalizane nao.

Fanja ni moja kati ya timu kongwe barani Asia ambapo Watanzania kadhaa wamewahi kuitumikia, mshambuliaji huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Yanga, Azam na Simba za Dar es Salaam alikuwa mbioni kurejea Yanga lakini ameamua kuikacha na kuelekea Oman, Mtandao huu unamtakia kila la kheri

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA