Mwinyi Haji Ngwali akana kutumia dawa za kulevya

Na Mwandishi Wetu

Beki wa kushoto wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Mwinyi Haji Ngwali amekanusha vikali kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya na anawashangaa wale wote waliokuwa wakimzushia.

Mwinyi ameshangazwa na watu waliokuwa wakimponda mitandaoni kwamba anatumia dawa za kulevya na ndio maana kiwango chake kilishuka, lakini mlinzi huyo amefichua kuwa kushuka kwa kiwango chake kulitokana na uchovu wa mwili na si madawa.

Hata hivyo beki huyo kwa sasa amerejea kwenye kiwango chake kama zamani na sasa amerejeshwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI