Simba yaipiga kidude kimoja Azam FC jana

Na Saida Salum, Dar es Salaam

Simba SC jana jioni ilijiongezea pointi tatu muhimu baada ya kuilaza Azam FC bao 1-0 katika mchezo mkali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliokuwa mgumu hasa kutokana na timu zote mbilj kuwa na upinzani mkali kila zinapokutana, hadi mapumziko Simba hawajapata kitu wala Azam inayonolewa na nakocha wa Hispania Zeben Hernanndez na msaidizi wake Jonas Garcia.

Azam iliyokuwa na washambuliaji wake John Bocco "Adebayor" na Ronaldo Ya Thomas bado walishindwa kuupenya ukuta wa Simba uliokuwa ukilindwa vema na Method Mwanjali na Novat Lufunga, Shiza Kichuya, Laudit na Ibrahim Ajibu waliongoza safu ya ushambuliaji ya Simba.

Lakini katika kipindi cha pili Shiza Ramadhan Kichuya akaipatia Simba bao la ushindi, Simba sasa iko kileleni ikiwa na pointi 13

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA