Mwaisabula afichua ya Serengeti Boys

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

Kocha wa zamani wa Bandari Mtwara, Ashanti na Yanga SC, Kenny Mwaisabula 'Mzazi' amefichua ya Serengeti Boys ya kutumia wachezaji vijeba mwaka 2004 na kuondoshwa na CAF kwenye fainali za mataifa Afrika zilizofanyika Gambia.

Akizungumza katika kipindi cha michezo cha MBS kinachorushwa kuanzia saa tano asubuhi mpaka saa saba mchana na redio Sibuka ya jijini Dar es Salaam, Mwaisabula amesema Serengeti timu ya umri wa miaka 17 lakini ilikusanya wachezaji waliozidi umri huo.

Mzazi aliwataja wachezaji kama Athuman Idd 'Chuji' , Mrisho Ngasa, Kiggy Makassy, Amir Maftah, Hassan Bwaza, Patrick Mangunguli, Nizar Khalfan, Nurdin Bakari, Yusuph Mgwao na David Mwantebe tayari walishazidi umri huo kwakuwa walianza kucheza Ligi kuu kabla hawaitwa timu hiyo ya vijana.

Mbali na Nurdin kugundulika, bado kulikuwa na wachezaji wengine anaowafahamu kudanganya umri ni wengi akiwemo Chuji na Mangunguli, 'Chuji alikuwa anaichezea Polisi Dodoma halafu akaitwa Serengeti, ina maana alianza kucheza Ligi kuu akiwa na miaka 16? mbona akuandikwa kwenye kitabu cha Guinnes kama mchezaji mdogo zaidi', anasema Mzazi ambaye kwa sasa ni mchambuzi.

Aidha kocha huyo wa zamani wa Yanga amesema hadi sasa hakuna mchezaji mwenye miaka 17 katika kikosi cha Serengeti Boys na wale waliopo ni wakubwa, amedai kwa sasa kuna uhaba wa wachezaji wenye umri kama huo kutokana na mazingira yenyewe huku akilalamikia ukosefu wa viwanja

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA