Tshabalala azawadiwa gari na Hanspoppe

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

Beki wa kushoto wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' ukipenda Zimbwe Jr amezawadiwa gari aina ya Ruum na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Klabu ya Simba, Zackaria Hanspoppe leo asubuhi.

Kiungo huyo wa ulinzi amezawadiwa gari hilo hasa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa akiwa na timu hiyo inayoshikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Tshabalala amekuwa katika wakati mzuri tangu alipojiunga na timu hiyo misimu miwili iliyopita, beki huyo alipiga krosi mbili zilizozaa magoli wakati Simba ikiifunga Ndanda FC mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu bara

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA