Ndanda yaikwamisha Yanga
Na Ikram Khamees, Mtwara
Yanga SC mabingwa wa soka Tanzania bara, wamejikuta wakikwamishwa na vijana wa Ndanda FC baada ya kulaximishwa sare tasa 0-0 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Vijana wa Ndanda walionekana kuwadhibiti vilivyo Yanga katika kipindi cha kwanza wakipeleka mashambulizi langoni kwa Yanga na kama si umahiri wa kipa Ally Mustapha huenda Yanga ingelala.
Hata hivyo Yanga itajilaumu wenyewr baada ya kukosa mabao ya wazi kupitia kwa washambuliaji wake Obrey Chirwa na Saimon Msuva, Yanga sasa imefikisha pointi nne ikiwa imecheza mechi mbili