Ngoma, Tambwe waendeleza moto Yanga ikiitwanga Mwadui kwao
Na Salum Fikiri Jr, Shinyanga
Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, jana jioni walicharuka baada ya kuichabanga bila huruma Mwadui ya Shinyanga mabao 2-0 mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.
Mwadui inayonolewa na Jamhuri Kihwelo "Julio" ilishindwa kabisa kuonyesha makeke yake kama iliyokuwa nayo msimu uliopita baada ya kukubali kipigo hicho mapema kabisa.
Mfungaji bora wa msimu uliopita Amissi Joselyin Tambwe akawa wa kwanza kuifungia bao Yanga na hadi mapumziko wakawa mbele kwa bao hilo, kipindi cha pili Yanga wakaongeza bao la pili lililofungwa na Donald Ngoma.
Goli hilo lilipatikana katika dakika za mwishoni kabla mpira haujamalizika, matokeo mengine, Tanzania Prisons na Mbeya City zilitoka sare 0-0, Mbao FC ikaichapa Ruvu Shooting 4-1, Ndanda FC ikaifunga Majimaji 2-1.
Mechi nyingine Simba ikailaza Azam 1-0, Mtibwa Sugar ikailaza Kagera Sugar 2-0 wakati leo hii Stand United inacheza na JKT Ruvu