Yanga kuendeleza mauaji Mtwara
Na Ikram Khamees, Mtwara
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Young Africans (Yanga) jioni wanashuka katika dimba la Nangwanda Sijaona mjini hapa kuwavaa wenyeji wao Ndanda FC mchezo wa Ligi kuu bara.
Licha kwamba Yanga itawakosa nyota wake muhimu kama Ally Mustapha 'Barthez', Vincent Bossou na Haruna Niyonzima 'Fabregas', lakini hata hivyo ina shehena ya wachezaji nyota na inaweza kurejea na ushindi.
Ndanda nayo ikiwa imejeruhiwa katika mechi mbili ilizocheza ikifungwa mabao 3-1 na Simba jijini Dar es Salaam, pia ikifungwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar Morogoro, haitakubali kuendelea kupoteza mbele ya Yanga ambao wamekuwa na rekodi mbaya kwenye uwanja huo wakicheza na Ndanda.
Hata hivyo Yanga ina kumbukumbu nzuri ikianza ligi kwa kishindo baada ya kuilaza African Lyon mabao 3-0 uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, safu ya ushambuliaji ya Yanga itaongozwa na mfungaji bora msimu uliopita Amissi Tambwe raia wa Burundi akisaidiana na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, wakati Ndanda itamtegemea Shija Mkina