Kiiza tayari kabisa kumrithi Ngasa Free State
Na Mwandishi Wetu
Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngasa akivunja mkataba wake na Free State, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Hamisi Kiiza tayari amejiunga na timu hiyo kuchukua nafasi ya Ngasa.
Kiiza aliyetupiwa virago vyake na klabu ya Simba ya Tanzania, amesajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja na Free State majuzi lakini imebainika amekwenda kuchukua nafasi ya Ngasa.
Kiiza ambaye aliwahi kuzichezea Yanga na Simba, amejiunga na timu hiyo akiwa na matumaini kibao ya kung' ara kwanj tayari alishafanikiwa kufunga mabao 19 katika timu yake ya mwisho kuichezea ya Simba katika Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara