Pan Africans waikana Yanga mchana kweupe, wasema hawana udugu nao

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwanachama wa Pan Africans FC ya Dar es Salaam, Abbas Ally Mwinyisimba, amesema Pan haina undugu na Yanga tofauti na watu wengi wanavyofahamu.

Akizungumza hayo jana, Mwinyisimba amedai Pan Africans imetokea ubavuni kwa Yanga baada ya kutokea mgogoro mkubwa mwaka 1976 uliopelekea Yanga Raizon na Yanga Kandambili ambapo ndipo mgawanyiko huo ukazaa Pan Africans ambayo haina undugu tena na Yanga.

"Hata mume akimuacha mkewe ndio basi tena huwezi kusema wana undugu, undugu ni pale wanapokuwa pamoja, sisi Pan hatuna undugu na Yanga isipokuwa tulitokea ubavuni mwao, hata Sunderland (Sasa Simba) nao walitokea ubavuni mwa Yanga lakini hawana undugu", alisema mwanachama huyo aliyekuwa akihamasisha wanachama wenzake kuudhuria mkutano mkuu unaofanyika leo Dar es Salaam.

Pan Africans iliwahi kuwa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara miaka iliyopita na ikawa moja kati ya timu tishio kwenye soka la Tanzania ikiwa na wachezaji mashuhuri kama Juma Pondamali 'Mensah', Jellah Mtagwa, Leodegar Tenga, Kassim Manara na wengineo

Mzee Abbas Mwinyisimba aliyevaa kofia akiwa na mtangazaji wa kipindi cha michezo redio Sibuka FM, David Pasko

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA