Kipre Tchetche akwama Umangani, sasa anaingoja Yanga mwakani
Na Mwandishi Wetu
Mfumania nyavu mwenye uwezo wa juu, Kipre Herman Tchetche hatimaye ameshindwa kuendelea kuichezea klabu ya Al Nahda ya Oman hasa baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kumalizana na Azam.
Taarifa zenye uhakika kutoka Oman zinasema kwamba mshambuliaji huyo aliyekuwa tegemeo katika kikosi cha Azam FC amerejea kwao Ivory Coast na hana mpango wowote wa kujiunga tena na Azam isipokuwa hesabu zake mwakani arejee nchini kujiunga na Yanga SC.
Yanga wanamsubiri kwa hamu Tchetche kwani walikuwa wakimuwania kwa kipindi kirefu isipokuwa viongozi wa Azam walikuwa hawako tayari kumuachia aende mitaa ya Jangwani na Twiga