Dante ajihakikishia namba Jangwani
Na Salum Fikiri Jr, Shinyanga
Kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Van der Pluijm, amesema ataendelea kumuamini katika kikosi chake cha kwanza, beki wake Vincent Andrew 'Dante' kama anavyomuamini kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Boniface Mkwasa.
Nyota ya Andrew Vicent 'Dante' inazidi kung'ara! Baada ya kucheza vizuri kwa dakika zote dhidi ya Nigeria akiitumikia Taifa Stars katika michuano ya AFCON,kocha mkuu Mkwasa amevutiwa mno na mchezaji huyo habari ni ile ile kwa kocha mkuu wa Yanga SC Hans Van Pluijm anayesema. .
"Ni kijana mwenye juhudi na nidhamu kubwa sana, anaongoza kuondoa mipira yote ya juu japo kiumbo sio mrefu. . Ntaendelea kumtumia na kumuamini, ana kipaji kikubwa sana atafika mbali kama ataendelea kuwa na nidhamu ya kipaji chake" alisema Pluijm