Ukata wairejesha Yanga Kaunda
Na Prince Hoza
Imebainika kwamba mabingwa wa soka nchini Yanga wameshindwa kuendelea kujifua kwenye uwanja wa Gymkhana au Boko Veteran baada ya mwenyekiti wao Yusuph Manji kukataa kulipia gharama kwa kile kinachodaiwa kukasilishwa.
Manji amekacha kulipia gharama za kukodi viwanja baada ya kukataliwa kwa ombi lake la kutaka kuikodi Yanga kwa miaka kumi na inadaiwa amesitisha mpango huo.
Pia baada ya Manji kususa, wachezaji wa timu hiyo bado hawajalipwa fedha zao na sasa wanacheza chini ya kiwango ili kutaka walipwe fedha zao, wakati hilo likiendelea, uongozi wa Yanga umejikuta ukiirudisha timu katika uwanja chakavu wa Kaunda kwavile hakuna uwezekano wa kufanyia mazoezi kwingine