Serengeti Boys yaiangamiza Congo Brazavile, lakini njia panda
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys jioni ya leo imeichakaza vibaya timu ya taifa ya Congo Brazaville mabao 3-2 uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa kufuzu fainali za mataifa Afrika.
Stars ilitangulia kupata mabao yake katika kipindi cha kwanza yakifungwa mapema kabisa mawili, hadi mapumziko Serengeti ilikuwa mbele, kipindi cha pili Serengeti iliongeza la tatu wakati Congo Brazaville wakajipatia mabao yao mawili.
Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Yohana Oscar Nkomola aliyefunga mawili katika dakika ya 43 na 45 kipindi cha kwanza, bao la tatu lilifungwa na Issa Abdi Makamba.
Magoli ya Congo Blazaville yamefungwa na Langa Lasse kwa mkwaju wa penalti baada ya Mbaungou Prastige kuchezewa rafu na Israel Patrick, goli lingine lilifungwa na Bopoumela Chardon katika dakika ya 88 akimalizia krosi ya Ntota Gedeon