Simba yamuuza kinyemela Danny Lyanga
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, inadaiwa imemuuza mshambuliaji wake Danny Lyanga kwa klabu ya Oman SC ya Oman inayoshiriki Ligi kuu nchini humo.
Hata hivyo, Mtendaji mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Patrick Kahemela amekataa vikali kuthibitisha hilo na kudai Lyanga hajauzwa isipokuwa ameenda Oman kufanya majaribio ma kama akikubalika anaweza kuuzwa.
Lakini mshambuliaji huyo aliondoka mwezi uliopita kujiunga na timu hiyo na sasa ni mchezaji wa Oman SC lakini haijulikani kama amesaini mkataba wa muda gani huku ikidaiwa Simba ilimuuza kinyemela.
Lyanga ni mmoja kati ya washambuliaji hatari waliofanya vizuri msimu uliopita akiwa na Simba sambamba na Ibrahim Ajibu, Hamisi Kiiza na wengineo