Kisa mataji, Ngasa aitosa Free State

Na Mwandishi Wetu

Mshambuliajj wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngasa ameamua kuvunja mkataba na klabu yake ya Free State Stars inayoshiriki Ligj kuu ya ABSA nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bethlehem Afrika Kusini zinasema kwamba Ngasa ameamua kuachana na Free State kwa kile kinachodaiwa kukosa furaha ya kubeba mataji.

Ngasa amesema Free State haina malengo na imekuwa ikipambana bila mafanikio, "Nataka kucheza timu yenye uwezo wa kunyakua mataji, karibu timu zote nilizowahi kucheza zimetwaa ubingwa", anasema Ngasa.

Ngasa ameweka mpango wake wa kutaka kujiunga na timu nyingine ambayo anadai ataitaja hivi karibuni, Ngasa amewahi kuzichezea Toto Africans, Kagera Sugar, Yanga, Azam na Simba, je atarejea Bongo?

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA