Simba yaipigisha kwata Polisi Dodoma

Na Ikram Khamees, Dodoma

Simba SC jana jioni imefanikiwa kuwapigisha kwata maafande wa Polisi Dodoma baada ya kuwachapa mabao 2-0 mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.

Simba wakicheza kandanda zuri na la uhakika ilifanikiwa kujipatia bao lake la kwanza katika kipindi cja kwanza lililofungwa na kiungo Abdi Banda.

Mabingwa hao wa zamani waliandika bao la pili katika kipindi cja pili lililofingwa na Said Ndemla, Simba imeamua kuelekea Dodoma na kucheza mechi ya kirafiki ikiwa kama kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe John Magufuli aliyehamua kuihamishia serikali yake Dodoma

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA