Yanga yaikandika Majimaji 3-0 yakamata nafasi ya pili

Na Prince Hoza

YANGA SC jioni ya leo imechupa kutoka nafasi ya saba hadi ya pili baada ya kuilaza Majimaji ya Songea mabao 3-0 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam mchezo wa Ligi kuu bara raundi ya tatu.

Yanga iliandika kalamu ya mabao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Donald Ngoma aliyemalizia kwa shuti kali mpira uliogonga mwamba uliotokana na penalti ya Simon Msuva.

Msuva alipiga penalti mara tatu, mbili akifunga na mwamuzi akikataa, na moja aligongesha mwamba na Ngoma kumalizia, Akaunti ya magoli iliendelea kipindi cha pili ambapo Amissi Tambwe alifunga magolj mawili na kuifanya Yanga ifikishe pointi saba ikiwa imecheza mechi tatu, kesho Simba itacheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI